16 Kristo Dhidi ya Ushirikina; Utajuaje Kama Jambo ni la Shetani au la Mungu? (Nyayo za Kristo)

9 Julai, 2025

Kitabu: 1 Timotheo

Bible Passage: 1 Tim 4:7, Isa 47:9-13

Ushirikina, uchawi, uaguzi, uganga na hata utabiri, Je hizi ni tamaduni au mwenendo hasi katika jamii? Na kama ni tamaduni au desturi zina mchango gani katika jamii zetu?

Mchungaji Mtende ameweza kutupa uzoefu wake juu ya haya mambo katika jamii kadha ambazo amewahi kutembelea . Ni kweli haya mambo yapo na kihalisia mchango wake si bora katika jamii kwani tumeona watu wakirogana na hata kurudishana nyuma kimaendeleo wengine wanaenda mbali kabisa wanaweza hata kuuana. Na kwa sababu haya mambo yapo tunazaliwa na kuyakuta yakihadithiwa au hata kufuatwa. Mchungaji Mtende anatuonesha maandiko yanatuelekeza nini juu ya jambo hilo kama Wakristo katika 1 Tim 4:7 “bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.”

Pia aliweza kueleza kwa upana juu ya mambo hayo kutoka katika Biblia kuanzia ushawishi wa hayo mambo, matokeo yake na hata hatima ya wanayoyafanya hayo Isa 47:9-13

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com