Fedha au mali ? Hivi ni vitu vinavyo wafikirisha sana watu wanaoanza safari ya kumfuata Kristo. Ni kweli katika dunia ya sasa tuna uhitaji wa hivi vitu ili shughuli zetu ziendelee. Mwalimu Smith anakubaliana na hilo kwa asilimia mia moja lakini haamini kwamba tunazihitaji hizo pesa kwa wingi kiasi kwamba hata kuzipata kwa njia isiyo ya halali au kwa kumkufuru Mwenyezi Mungu, na anatupa angalizo juu ya mali na pesa kutoka katika maandiko matakatifu 1 Tim 6:9 “Lakini hao watakao kua na mali huanguka katika majaribu na mitego, na tamaa nyingi zisizo na maana , zenye kudhuru, zinazowaingiza watu katika upotevu na uharibifu.” Ni kweli alipata maswali wakati wa somo lakini hakuona ajabu juu ya maswali hayo juu ya mishangao akatukumbusha hata Yesu alipozungumza haya wanafunzi wake walihamaki sana na akateuleza Yesu alivyowaambia Mat 19:23-25.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com