14 Kristo Dhidi ya Michezo; Mkristo Anaweza Kuwa Mshabiki wa Mpira? (Nyayo za Kristo)

19 Juni, 2025

Kitabu: 1 Timotheo

Bible Passage: 1 Tim 4:8, Rum 12

Michezo ni burudani. Sawa lakini swali ni Je! watu wanaburudikaje na hiyo michezo? Mchungaji Mtende anaeleza kwa ufasaha juu ya jambo hilo uku akiwa na uchungu moyoni mwake, kutokana na jinsi jamii ya leo inamsahau Mungu na kumezwa na burudani. Anakiri wazi kwamba hata zamani watu walikua wakijihusisha na michezo na washindi walipewa zawadi. Ila ni tofauti sana na michezo ya sikuizi kama mipira, ndondi, na hata miziki kwani katika michezo hiyo sikuhizi kumekua na ushindani wa mizaha ya hali a juu, ubashiri na hata ushawishi mkubwa kupelekea watu wengi kuipa kipaombele zaidi kuliko hata shughuli za kiroho ikiwemo ibada. Na anarejea katika Biblia kutukumbusha juu ya jambo hili Mat 6:24 “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu ,na kumpenda huyu; ama atashikamanana huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. Aliyasema yote hayo kwa sababu alikua akifundisha juu ya Nyayo za Kiristo na kutukumbusha juu ya michezo kwani watu wengi wameifanya michezo kua bwana wao na kumsahau Bwana wetu Kristo na nyayo alizotuachia tuzifuate.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767