13 Kristo Dhidi ya Zinaa; Zinaa ni Nini? Na ina Madhara Gani? (Nyayo za Kristo)

16 Juni, 2025

Mada: Usafi, Uzinzi

Kitabu: Mithali

Bible Passage: Mith 23:26-27

Zinaa ni nini? Hili ni swali ambalo huibua hoja nyingi katika fikra za watu tofauti tofauti kutokana uelewa wao , lakini katika somo hili ndugu Jeff ameweza kutuelezea kwa ufasaha kwamba zinaa ni kitendo cha mwanamume na mwanamke kukutana kimwili ingalikua sio wanandoa. Pia hakuishia hapo tu aliweza kutukumbusha kwamba hakuna zinaa pasi na mawazo juu ya zinaa kichwani kwa mtu. Na akatueleza Kiristo alivyozungumza juu ya suala hilo katika biblia, Mt 5:28 “lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Na aliweza kutoa mifano mingi kama Samsoni na Delila kutoka Amu 16:20 na wosia wa mamake na Suleimani juu ya wanawake Mit 9:13-17. na licha tu ya kwamba zinaa ni dhamdi pia zinaa ni chanzo kikuu cha maradhi ya kuambukiza katika jamiii pia kua sehemu ya ongezeko la watoto wa mitaani, kama alivyotukumbusha ndugu Jeff kutoka Mith 6:27 “Je! mtu aweza kuchukua moto kifuani pake,na nguo zake zisiteketezwe?

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767