09 Kristo Dhidi ya Uongo; Kuna Wakati Unaofaa Kutumia Uongo? (Nyayo za Kristo)

3 Machi, 2025

Kitabu: Efeso

Nani ni Baba wa Uongo? Katika Yoh 8:44 tunajifunza kwamba ni Ibilisi. Nani ndiye Kweli? Katika Yoh 14:6 tunakuta kwamba ni Yesu. Sasa kama wanafunzi wa Yesu tutaweza kusemo uongo? Ungana nasi katika somo hili pamoja na kaka Mikael akifundisha umuhimu wa kusema ukweli. Kuna mifano mbalimbali inayoonyesha kuwa tukisema uongo watu hawatoweza kutuamini. Halafu pia Biblia inasema kwamba waongo wote watukuwa na sehemu yao katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Ufu 21:8 Tuwe watu wa kuzungumza tu yaliyo kweli. Amina

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767