36 Kristo na Mali; Pesa Ulizonazo ni ya Nani? (Nyayo za Kristo)

19 Novemba, 2025

Kitabu: Luka

Bible Passage: Luka 12:20

Mali kwa ujumla yaweza kuwa ni fedha, nyumba, gari, dhahabu, mashamba na vitu vingine vyenye thamani ambavyo vyaweza kuhamishika au kutohamishika, vinaweza kuwa vya urithi ama umevitafuta kwa jasho lako mwenyewe.

Lakini katika somo hili Mch Koroso ameweza kutueleza kuwa hivyo vitu ni vya nani na nani ni mmiliki mkuu japo mara nyingi vinakua vipo mikononi mwetu kama mawakili. Alieleza pia kuwa wakili ni nani.

Lengo la somo hili hasa Mch Koroso anatusihi sisi kama wafuasi wa Kristo kuwa makini sana juu ya hizi mali pale tunapopewa jukumu la uwakili na mwenyezi Mungu ambaye mali na vitu vyote ni vyake, na tusije kujisahau na kuona kama sisi ndio tunavimiliki na kwamba tunaweza kufanya lolote juu ya hizo mali kwa matakwa yetu bila mapenzi ya Mungu.

Aliweza kutupatia hadithi ya kijana mpumbavu kutoka katika maandiko na kutusihi sisi kama wakristo tusiwe mfano wa huyo kijana pale Mungu anapotupa uwakili, yatupasa tumtukuze yeye na sio kujitukuza sisi kwa hizi mali alizotupatia. Na alituonesha Mungu atatujibu nini endapo hatutakuwa wanyenyekevu na wenye kumtukuza baada ya kutupatia mali.

” Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? ” (Luka 12:20)

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com