35 Kristo na Elimu; Wakristo Wanatakiwa Kuwa na Elimu Tofauti na Watu wa Dunia? (Nyayo za Kristo)

19 Novemba, 2025

Kitabu: Mithali

Bible Passage: Mithali 1:7

Elimu ni nini na lipi ni lengo lake? Zipo tafsiri nyingi kuhusu elimu, lakini huu ni mchakato wa kupokea, kuendeleza, au kueneza maarifa, ujuzi, maadili na mwelekeo wa tabia kwa kujifunza kwa njia rasmi au isiyo rasmi. Lengo lake kubwa ni kuongeza uelewa kwa ambaye hakua na huo uelewa.

Mchungaji Tim katika somo hili anakubaliana na hii tafsiri juu ya elimu lakini amesisitiza sana umuhimu wa hekima ya Mungu katika kila tunalojifunza katika elimu , na ameweza kutofautisha kati ya hekima ya Mungu na hekima ya wanadamu.

Pia ameweza kutoa tahadhari kwa wazazi ambao hawazingatii misingi ya kimungu katika kuwachagulia watoto wao shule za kwenda kusoma. Na umuhimu wa kuzingatia misingi ya kimungu pia. Ameweza kutoa mifano mbali mbali kuhusu eneo hilo.

Mwisho anasisitiza vyovyote vile tutakavyoitafuta elimu ya hapa duniani kwa sababu mbali mbali tusisahau kwamba “Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa” (Mithali 1:7)

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com