Utakatifu ni nini? Hii ni hali ya ubora usioelezeka katika usafi usio na dosari yeyote kimwili au kiroho. Somo lililopita tuliangalia zaidi kuhusu familia na sasa tunaangalia usafi au utakaso ambao unatakiwa kudumishwa ndani ya familia.
Katika somo hili mwalimu Smith ameweza kutufundisha mambo mengi yatupasayo kuyafanya kama wazazi katika familia ( kwa watoto wetu) kama kupendana kwa dhati mbele yao , pia kuwa makini na marafiki zao, kujua wanavyovitazama na hata lugha wanazotumia. Na hakuishia hapo aliweza pia kutueleza namna sahihi ya kudumisha utakatifu katika familia kwa jitahada zetu kama wazazi na sio mchungaji , jilani wala mwalimu mwenye jukumu hilo juu ya familia ambayo Mungu amekupa kama zawadi.
Na alikukumbusha juu ya tahadhari ambayo biblia Inatupatia endapo hatutakua makini katika jambo hilo.
“Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze. “(1 Petro 5:8)
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com
