Mtoto ni nani? Ni kiumbe kisicho na hatia wala hakijui chochote kuhusu hii dunia na huletwa na Mungu kwetu kama zawadi, na jukumu letu linabaki ni kumpenda , kumlinda, kumtunza na kumfundisha mazuri ambayo yatakua msaada pale atakapokua mtu mzima. Kwa tafsiri hii inamana kuwa hakuna ambaye hakuwahi kuwa mtoto.
Mch. Mtende naye analikubali hili, lakini katika somo hili anaonesha kuumizwa na baadhi ya kauli ambazo anazisikia kutoka kwa watu wazima na vijana ambao nao mwanzo walikua watoto.
Wapo ambao wanasema watoto ni usumbufu, wengine wanasema watoto ni gharama wao hawana pesa za kuwamudu na wengine husema kabisa hawataki watoto.
Na wanayesema hayo bila kukumbuka kwamba watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu kwani wapo hata wanandoa ambao hawajapata hiyo zawadi. Mch. Mtende anawasititiza hao wasifadhahike bali watumie iyo nafasi kwa watoto ambao ni yatima.
Amefundisha mengi mazuri nakutueleza maandiko yanatuagiza nini juu ya watoto ” Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu. Kama mishale mkononi mwa shujaa, ndivyo walivyo watoto wa ujanani.” (Zaburi 127:3-4)
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com