Je! adui ni nani? Wengi wetu tunaamini ya kwamba adui ni mtu au watu ambao mara zote wapo kinyume juu ya mema yako, hata kukudhamilia mabaya kwa ajili yako. Na kikubwa zaidi katika somo hili ndugu Patrick anatufundisha kwa mapana na kina kwamba hao madui wanaweza kua ni mama yako, baba yako, dada, kaka, hata mume au mke wako wa ndoa. Na katika somo hili anatufundisha ni jinsi gani ya kuishi na hao maadui kwa upendo, tukiwa kama sisi ni wafuasi wa Kristo. Pia ametukumbusha maneno ya Yesu alipokua pale mlimani ni nini alisema juu ya hilo Mat 5:38-48. Yesu alisisitiza kwamba tuwapende wanaotuudhi kwani hakuna faida ya kuwapenda ambao wanatupenda. Kwani tukifanya kama hivyo hatutakua na utofauti na watu wa mataifa , ambao wao huwasalimia wanaowasalimia na kuwajali wanaowafurahisha.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com