Anasa ni nini?, Na inamchango gani katika kutuangusha au kutupoteza katika mihimili yetu ya kiroho sisi waamini katika kiristo?
Ndugu Tim ameeleza kwa upana kuhusu anasa na vyema zaidi anatufahamisha kuhusu nani anayenaswa katika anasa.
Kihualisia anasa zote ninazo zifahamu ni kwa ajili ya kuburudisha mwili (hivyo binadamu wengi huvutwa nayo) lakini mara nyingi mwisho wake ni kuharibu mwili mfano pombe, sigara, wanawake na hata kucheza miziki na kwa kulielewa hilo Ndugu Tim anatukumbusha jukumu letu juu ya miili yetu kutoka katika Biblia 1 Kor 6:20 “Kwa maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767