Neno la Mungu linasema: “Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.” (Waefeso 4:29) Bila shaka maneno yetu yana umuhimu. Kwa mazungumzo yetu tunaweza kubomoa au kujenga. Tunawezaje kudhibiti ulimi wetu? Maana Biblia inasema: Yak 3:8 “Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.” Wanadamu wameweza kufuga wanyama wakali wa porini lakini ulimu ni ngumu sana kuuweza. Kama waswahili wanavyosema “Ulimu hauna mfupa.” Tufanyeje basi tuweze kuwa watu wanaompendeza Mungu katika maongezi yetu? Karibu katika somo hili pamoja na ndugu Jeff. Utaweza kujifunza kuhusu hatari ya kuwa na maneno mengi, maneno machafu, mizaha, na masengenyo. Mungu atusaidie kuwa na maneno yanyofaa na siyo ya kuharibu.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767